AMTOA MWANAE ILI ALIWE NA FISI

Jeshi la
Polisi mkoani Simiyu linamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha Songambele
wilayani Maswa, kwa tuhuma za kutaka kumuua mtoto wake kwa kumtupa na
kumtelekeza nje ya nyumba ili aliwe na fisi.
Kamanda wa
polisi mkoani Simiyu, Charles Mkumbo alisema ofisini kwake jana kuwa
tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nane usiku wakati mtuhumiwa Baya
Seni (30) akiwa amelala na familia yake kijijini hapo, ndipo
alipokurupuka ndani akampiga mtoto wake Amos Baya (3) na kisha kumtupa
na kumtelekeza nje ya nyumba.
Alisema,
Seni katika maelezo yake kituo cha polisi alisema alifikia uamuzi huo
kwa kuwa hakuona thamani ya mtoto wa kiume kwenye familia yake kwani
uzoefu umeonesha kuwa watoto wa kiume wakikua hudai kupata mirathi
kutoka kwa wazazi wao .
Alisema
kinyume chake watoto wa jinsia ya kike wakikua watamuongezea utajiri wa
mifugo atakapolipwa mahari ili waolewe na baada ya kuolewa hawawi mzigo
tena kwenye familia yake bali mzigo huo huhamia kwenye familia
atakayoolewa. Mtoto huyo aliokolewa na majirani baada ya kusikia kilio.
No comments:
Post a Comment