50 Cent na mapenzi yake, amesemaje kuhusu kuwa na msichana kama Rihanna?
Kama hii ilikupita ni kwamba rapper 50 Cents ameeleza sababu ya kutokuweza kuwa na mwanamke kama Rihanna kwenye interview na show ya The rickey smiley ambapo pia amezungumzia kwanini mapenzi yake na Wanawake tofauti hayakudumu.
Kuhusiana na mapenzi yake yaliyopita na mwigizaji Vivica A. Fox, 50 anasema ilikua ni penzi la haraka yaani kama ajali manake haikua imepangwa na alikua akizongwa na kazi nyingi mpaka kufikia mwisho wa uhusiano huo.Anasema “ni hizi safari za kazi (tour) zilikua zikitupeleka sehemu tofauti hivyo ilikua ni nafasi nzuri ya sisi bado kupendana lakini kama mmekuwa mbali muda mrefu, yeye hatofurahia hilo na mwisho itashindikana”

Alipomzungumzia Rihanna, 50 amesema kamwe hawezi kuwa na mwanamke kama Rihanna kwa sababu RiRi ana mambo yake, anapoweza anaachana tu na mwanamme na inaonekana kama Mwanaume alikua na Wanawake wengine, yaani anajiumiza…mtu mwengine kama Rihanna ni Erykah Badu, wako tofauti tu.. mi sitaki mwanamke aina hiyo, mwanamke aina gani sasa hii”

No comments:
Post a Comment