Wednesday, 30 April 2014


DUUUUUUUH HII SASA NAYO KALI KAMA UJAWAHI SIKIA KITUKO HIKI NI KITUKO TENA SI KIDOGO MTOO WA MIEZI TISA AMBAYE HATA KUNYANYUA CHUPA YAKE YA MAZIWA HAWEZI ANATAFUTWA NA POLISI HUKO PAKISTANI KWA KOSA LA MAUAJI......UNATAKA KUJUA KAUA NINI INGIA NDANI USOME VIZURI....................


Mtoto wa Miezi Tisa Ashitakiwa Kwa Jaribio la Mauaji Pakistani

Mtoto wa miezi tosa (9) mafichoni kule LAHORE Pakistan kwa sababu ana kesi ya kujibu. Mtoto huyo pichani ambaye hata hawezi kunyanyua chupa yake ya maziwa anadaiwa kushiriki kwenye jaribio la mauaji.
Baby huyo anayeitwa Musa Khan sasa yuko mafichoni kwani polisi wanamtafuta. Wiki iliyopita mtoto huyo alipelekwa mahakamani na kutajiwa kesi hiyo ya jaribio la mauaji katika mojawapo ya mahakama mjini LAHORE.
Pamoja na mtoto huyo Baba yake na Babu yake wanahukumiwa pia. Sakata hilo lilianza pale polisi mmoja na mfanyakazi wa kampuni moja ya gesi aliyekuwa anakusanya bili za muda mrefu waliporushiwa mawe na waandamanaji wanaopinga kupunguzwa kwa gesi na kupandishwa bei.
Kesi ya kichanga hiki inaonyesha wazi udhaifu ulioko kwenye sheria za PAkistani
Hata hivyo taarifa za hivi punde kutoka LAHORE, Pakistani zinasema kuwa mahakama hiyo imemfutia kesi mtoto huyo

No comments:

Post a Comment